1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yatolewa Euro 2016

Admin.WagnerD17 Juni 2016

Timu ya Ukraine imekua timu ya kwanza kuondolewa katika michuano ya soka ya kuwania ubingwa wa Ulaya inayoendelea Ufaransa wakati mashabiki kadhaa wakitiwa mbaroni kwa uhalifu mjini Cologne, Ujerumani

https://p.dw.com/p/1J8fY
UEFA EURO 2016 Ukraine - Nordirland *** Tor Nordirland
Mchezaji wa Ukraine katika mchuano wa Euro 2016Picha: Reuters/R. Pratta

Tukianzia na tukio hilo la kujeruhi, watuhumiwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 26 na 30 walisimama kwa muda mjini Cologne baada ya kuondoka eneo la Marseille, ambako kulikuwa machafuko mabaya kabisa kuwahi kutokea katika mashindano ya kimatiafa tangu 1998 wakati wa mchuano wa Kombe la Dunia. Vurugu zilizuka Jumamosi iliyopita wakati Urusi ilipochuana na England.

Watano mbaroni mjini Cologne

Katika tukio hilo lililotokea jana Alhamis, polisi ya hapa Ujerumani inasema vijana hao walikuwa wakifanya vitendo vya karaha na vibaya dhidi ya watalii watatu wa Kihispania. Wakielezea pasipo kutaja chanzo cha kuzusha vurugu hizo, polisi walisema mashabiki hao wa soka wa Kirusi, waliwapiga wahanga na kumwacha mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya.

Deutschland Köln Blaulicht der Polizei vor Kölner Dom
Picha: Imago/Eibner

Hata hivyo, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano miongoni mwao katika eneo la tukio na huku mmoja akitoroka. Wote walikuwa katika maandalizi ya kuondoka nchini hapa kuelekea Urusi kwa usafriri wa ndenge na polisi wa Ujerumani imesema itawasiliana na Ufaransa ili kuweza kuhakiki kama hawakujihusisha na vitendo kama hivyo katika vurugu zilizojitiokeza katika mchuano wa Euro 2016.

Watatu wafungwa Ufaransa

Hapo jana Ufaransa iliwatupa gerezani mashabiki watatu wa Urusi katika mashindano hayo ya Euro 2016, kutokana na machafuko huku ikiwatimua nchini humo Warusi wenye mrengo mkali wa kulia.

Na katika michezo iliyofanyika jana, Ukraine imekuwa timu ya kwanza kuaga mashindano ya Euro 2016 na kocha wake Mykhailo Fomenko anatajawa kuwa atalipwa ujira wa kile alichopanda kwa maana ya kwamba kocha huyo mkongwe huenda akajizulu. Timu yake ilichapwa mabao 2-0 na Ireland ya Kaskazini huku England ikiivuruga Wales mabao 2-1.

Lakini mabingwa wa dunia tumu ya Ujerumani ililazimishwa sare ya bila kwa bila na Poland. Ukraine ambayo tayari ina tikiti ya kuondoka katika mchuano huo Jumanne ijayo itachuna na Poland, ukiwa mchezo wa mwisho kwa kocha Fomeko mwenye umria wa miaka 67, ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa mashindano hayo.

Leo hii mchunao unaendeleo ambapo Italia itachuana na Sweden, Uhispania na Uturuki wakati Jamhuri ya Czech itakwana na Croatia.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohamed Khelef AFP/DPA