1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yajadiliana udhibiti wa mipaka ya nje

3 Februari 2022

Mawaziri wa mambo ya ndani wa umoja wa Ulaya wamejadiliana namna ya kuimarisha usalama kwenye mipaka yake na mageuzi yanayohitajika katika mfumo wa ukimbizi wa Umoja wa Ulaya wenye matatizo makubwa.

https://p.dw.com/p/46Tbn
Belarus Grenze zu Polen | Migranten | Zuspitzung der Lage
Picha: Leonid Shcheglov/BelTA/AP/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya hii leo wamejadiliana namna ya kuimarisha usalama kwenye mipaka yake, ikiwa ni pamoja na kujenga uzio ama kuta zilizofungwa umeme lakini pia kuangazia kwa mara nyingine jinsi ya kuanzisha mjadala wa muda mrefu wa mageuzi yanayohitajika sana katika mfumo wa ukimbizi wa Umoja wa Ulaya wenye matatizo makubwa. 

Wasiwasi wa usalama wa mataifa hayo, mawimbi ya uhamiaji na zaidi janga la hivi karibuni la corona vimechangia pakubwa kurejeshwa kwa udhibiti wa mipakani katika eneo la Schengen na ukosoaji wa namna udhibiti huo unavyofanyika umefuta kabisa kile kilochotajwa kama mafanikio makubwa yaliyofikiwa Ulaya, katika kipindi cha baada ya vita vikubwa viwili vya dunia.

Soma Zaidi: Miaka mitano tangu maelfu ya wakimbizi walipoingia Ujerumani

Frankreich Kandidatinnen und Kandidaten BG Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anaona kuna umuhimu wa kuundwa chombo kipya cha kusimamia masuala kadha wa kadha ya Ulaya.Picha: Bertrand Guay/AFP/Getty Images

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, alipozungumza katika mkutano wa mawaziri wa sheria na mambo ya ndani wa Ulaya kaskazini mwa Ufaransa, amependekeza kuundwa kwa chombo alichokipa jina "Halmashauri ya Schengen" ambacho amesema kitakuwa na uwezo wa kutathmini kile kilichokuwa kikifanyika kwenye eneo hilo na kufanya maamuzi ya pamoja lakini pia kusaidia uratibu kunapotokea mzozo.

Amesema jana Jumatano kwamba chombo hicho kitakuwa ni kama kioo cha Ulaya thabiti na imara yenye uwezo wa kudhibiti mipaka yake na kwa maana hiyo, mustakabali wake utakuwa salama. Mkutano wa uzinduzi huenda ukafanyika wakati mawaziri hao wa ndani na sheria watakapokutana tena Machi 3, amesema Macron.

Pendekezo la Macron laungwa mkono na Ujerumani na Ulaya.

Mapema leo, waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin amesema kwenye mkutano huo kwamba upo umuhimu mkubwa wa kulinda mipaka ya nje ya Schengen, wakati akiwaalika mawaziri wenzake kwenye mkutano huo usio rasmi unaofanyika Lille, ikiwa ni siku moja baada ya rais Macron kupendekeza kuhusu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo ya Schengen.

Alisema "Ili kulinda raia wetu, na hapa naamanisha kwamba kuwalinda dhidi ya vitendo vya kigaidi vinavyoweza kufanywa na wahamiaji wanaotoka nje ya Umoja wa Ulaya, tunatakiwa kulinda mipaka yetu ya nj, iama iwe ya Hungary, Lithuania, Uhispania ama Ufaransa na kwa maana hiyo sote tunahusika. Si vibaya kukubaliana kuhusu usalama kwa wenzetu wa Ulaya, tunataka tu kuwa na mipaka ya nje ya pamoja. Kutokuwa tena na mipaka ya ndani inamaanisha kuwa tuna mipaka ya nje ya pamoja. "

Soma Zaidi: Umoja wa Ulaya wajipanga kwa wimbi la wakimbizi wa Afghanistan

Polen-Belarus-Grenze | Migranten  in einem Flüchtlingslager
Baadhi ya watoto wa wahamiaji wakiwa natizamana na wanajeshi wanaolind mpaka wa Belarus na Poland.Picha: Henadz Zhinkov/XinHua/dpa/picture alliance

Pendekezo kama hilo la Macron litatakiwa kuungwa mkono na wanachama wengine wa Umoja huo ili kuanza kufanya kazi, na maafisa wa Ufaransa wanasema halitabadilisha kwa namna yoyote mkataba wa Umoja wa Ulaya.

Ujerumani kupitia waziri wake wa mambo ya ndani Nancy Faeser imesema wanaunga mkono pendekezo hilo la Ufaransa na kamishna wa Ulaya wa mahusiano ya ndani Yvla Johansson naye akilikaribisha pendekezo hilo akisema wanahitaji sana kuimarisha usimamizi katika masuala ya siasa kwenye eneo hilo la Schengen. Mataifa mengine hata hivyo bado hayajatamka lolote.

Schengen ni eneo kubwa kabisa ulimwenguni la nchini 26 ambalo wakazi wake husafiri bila ya kuhitaji pasi, lakini limegawanyika kwa miaka kadhaa juu ya namna ya kushughulikia mzozo wa wahamiaji na udhibiti wa mipaka yake ya nje. 

Mashirika: APE