1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya yajitayarisha kufungua tena shughuli za kawaida

20 Aprili 2020

Mataifa yaliyoathiriwa vibaya na virusi vya corona barani Ulaya yanajitayarisha kuanza kufungua shughuli za umma huku mji wa New York nchini Marekani ukitangaza kupiga hatua muhimu kukabiliana na virusi vya va corona. 

https://p.dw.com/p/3b9do
Spanien Coronavirus | Madrid neues Risikogebiet
Picha: picture-alliance/ZUMAPRESS/J. Sanz

Bara la Ulaya limeshuhudia dalili za kutia moyo baada ya Italia, Uhispania, Ufaransa na Uingereza kuripoti idadi ndogo ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona siku ya Jumapili.

Hadi sasa bara hilo ndiyo limerikodi karibu theluthi mbili ya vifo 165,000 vya ugonjwa wa COVID-19 vilivyotokea duniani wakati maambukizi ya virusi vya corona yamepindukia visa milioni 2 na laki 3 leo Jumatatu

Ushahidi wa kitaalaum umethibitisha hatua za kujitenga na vizuizi vilivyowekwa vinapunguza kusambaa kwa virusi vya corona na hali hiyo imechochea mipango ya mataifa mengi kuanza kulegeza marufuku zilizowekwa na kufungua tena shughuli za kawaida.

Uhispania moja ya taifa lililoathiriwa vibaya limerefusha viuzizi vyake kwa nchi nzima lakini imesema itaanza leo kuwaruhusu watoto kutoka nje.

Nchi hiyo ilitangaza vifo 410 siku ya Jumapili, ambayo ni idadi ndogo kabisa ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita na maafisa wa afya wamesema rikiodi hiyo inatoa matumaini.

Mamlaka nchini humo wameanza kuyafunga maeneo kadhaa yaliyotengezwa haraka kukabiliana na wimbi la virusi vya corona ikiwemo eneo la kuhifadhi maiti katika uwanja wa michezo ya kwenye barafu mjini Madrid.

Mataifa mengine pia yatafungua shughuli za umma 

Dänemark Coronavirus Schulunterricht Mette Frederiksen
Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederiksen (wa pili kushoto) alipowatembelea wanafunzi baada ya shule kufunguliwaPicha: Getty Images/AFP/Ritzau Scanpix/P. Davali

Uswisi, Denmark na Finland zote zimetangaza kuyafungua tena maduka pamoja na shule zote kwenye mataifa hayo.

Ujerumani leo itaruhusu baadhi ya maduka kufunguliwa tena baada ya kutangaza kuwa imefanikiwa kudhibiti viruis vya corona huku Italia yenyewe ikijikongoja kuchukua hatua za kufungua tena shughuli za kawaida.

Iran, taifa linalokabiliwa na mlipuko mbaya kabisa wa virusi vya kaitka eneo la mashirki ya kati siku ya Jumamosi ilianza kuruhusu kufunguliwa biashara zilizo kwenye kiwango cha chini cha hatari ya kueneza ugonjwa wa COVID-19.

Nchini Marekani - taifa lenye idadi kubwa ya vifo na maambukizi ya virusi vya corona- gavana wa jimbo la New York Andrew Cuomo amesema mlipuko huo unaelekea kupungua ijapokuwa ametahadharisha bado ni mapema kuanza kujipongeza.

Baada ya wiki kadhaa za mivutano na serikali kuu mjini Washington kuhusu wajibu wake kwenye janga la corona, gavana Cuomo jana alitumia matashi laini na kusifu ushirikiano kati ya serikali kuu na majimbo kwenye mafanikio yanayoonekana.

Hata hivyo Marekani imeshuhudia maandamano ya mwishoni mwa juma ya kupinga vizuizi vilivyowekwa kukabiliana na viruis vya corona.

Waandamanaji katika majimbo ya Colorado, Texas, Maryland, New Hampshire na Ohio walikusanyika kupinga viuzizi hivyo wakisema vinaharibu uchumi na kusabaisha ukosefu wa ajira.

Rais mpinga vizuizi dhidi ya corona 

Brasilien | Jair Bolsonaro spricht vor dem Hauptquartier des Militärs | Brasilia
Rais Jair Bolsonaro wa BrazilPicha: Reuters/U. Marcelino

Hata hivyo hali ni tofauti nchini Brazil, taifa lenye idadi kubwa ya maambukizi katika eneo la Amerika ya Kusini.

Hapo jana rais Jair Bolsonaro wa nchini hiyo alijiunga na mamia ya waandamanaji nje ya makao makuu ya jeshi mjini Brasilia kupinga amri ya kubakia nyumbani iliyotangazwa na magavana wa majimbo nchini humo.

Rais Bolsonaro aliwaambia waandamanaji kuwa amejiunga pamoja nao kwa sababu anakubaliana na mawazo wanayotoa .

Mara kadhaa kiongozi huyo amekosoa hatua zilizochukuliwa na magavana za kuweka vizuizi vya wastani ikiwemo kwenye miji yenye idadi kubwa ya watu ya Sao Paulo na Rio de Janeiro ili kuzuia kusambaa virusi vya corona.

Mwandishi: Rashid Chilumba /AFP

Mhariri: