Ulaya yashutumiwa kwa unyanyasaji kwa wahamiaji wa Afrika
22 Mei 2024Uchunguzi uliofanywa na kundi hilo linalovijumuisha vyombo vya habari vya Le Monde na The Washington Post, umeutaja Umoja wa Ulaya kushirikiana na mataifa hayo ya kiafrika katika mpango wa uhamishaji wa watu wengi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Ripoti ya vyombo hivyo imesema Ulaya inaunga mkono, inafadhili na kuhusika moja kwa moja na operesheni ya kuwaweka kila mwaka maelfu ya wahamiaji weusi jangwani au katika maeneo yasiokuwa na watu ili kuwazuwiakufika katika mataifa ya Umoja huo.
Operesheni hizo zinadaiwa kufanywa kutumia fedha, magari, vifaa, habari za kijasusi na maafisa wa usalama kutoka Ulaya na Mataifa kadhaa ya Umoja huo. Msemaji wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Eric Mamer alipoulizwa kuhusu ripoti hiyo alisema inatoa hali ngunu na bado uchunguzi unaendelea.