Umaarufu wa Jürgen Klopp akiwa na Dortmund
Limefanyika, mashabaki wa Bundesliga. Kocha mkuu wa Borussia Dortmund Jürgen Klopp ataihama klabu hiyo mwishoni mwa msimu. Imekuwa miaka saba ya furaha kwa mashabiki wa BVB
Sura tuliyokuwa tumeizoea
Jurgen Klopp aliwasili katika mkutano wake wa kwanza wa waandishi wa habari katika klabu ya Borussia Dortmund mwaka wa 2008 akiwa na tabasamu kubwa. Matarajio hayakuwa makubwa mno, lakini historia iliyoandikwa na Klopp wakati akiwa na Borussia Dortmund itabakia milele katika vitabu vya historia ya kandanda la Ujerumani
Ushindi wa kwanza
Jürgen Klopp aliiweka kileleni mwa kandanda la Ujerumani klabu iliyokuwa ikiyumba, wakati wa uongozi wake wa miaka saba. Ushindi wake wa kwanza ulikuwa ni kuwazidi nguvu miamba Bayern Munich. Ushindi wa taji la Bundesliga mwaka wa 2011 yalikuwa mafanikio ya kwanza ya BVB kwenye ligi katika mwongo mmoja na yalikuwa mwanzo wa enzi ya kufana kwa klabu hiyo
Mafanikio yake makubwa kabisa
Jürgen Klopp aliiongoza Borussia Dortmund kunyakua mataji matatu katika uongozi wake wa miaka saba. Kwa mashabiki wengi wa BVB, mafanikio makubwa kabisa ya Klopp yalikuwa ni kuiongoza Borussia Dortmund kushinda mataji mawili: Bundesliga na Kombe la DFB Pokal mwaka wa 2012. Kuwapiku Bayern Munich katika vinyang’anyiro hivyo viwili kuliwapa utamu zaidi mashabiki wao
Klopp hakuwahi kuficha hisia zake
Jürgen Klopp hakuwa mtu wa kuficha hisia zake wakati wa michuano – kila mara alikuwa akipiga kelele, kukimbiana kushangilia kama mchezaji. Klopp alikuwa shabiki, na alifurahia sana kuonyesha katika matukio ya ushindi alioupata na timu yake ya Dortmund. “Mimi ni mtu mwenye hisia sana, na klabu hii ina umuhimu mkubwa kwangu” alisema mapema mwaka huu
Hatua moja kutoka juu
Baada ya mafanikio ya Bundesliga, Klopp alisalia tu na dakika 90 kuitawala Ulaya katika mwaka wa 2013. Mwishowe, kushindwa katika fainali ya Champions Leauge uwanjani Wembley na Bayern Munich kulikuwa na matokeo yake. Tangu wakati huo, Bayern wametawala kandanda la Ujerumani. Ilikuwa mara ya pili pekee kwa Dortmund kushiriki katika dimba hilo kubwa zaidi la vilabu na Klopp ndiye aliyekuwa fundi.
Mpenzi wa mashabiki
Jürgen Klopp hakupokea sifa tu kutoka kwa mashabiki kutokana na mafanikio yao, ilikuwa mtindo na ujasiri uliodhihirishwa na kocha huyo mkuu aliyevaa sare za michezo ambavyo viliwafanya mashabiki kote ulimwenguni kumpenda. Kinaya ni kuwa, msimu huu Klopp alikuwa kocha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya Dortmund, na pia mwenye mafanikio makubwa zaidi.
Dortmund-Bayern upinzani uliofufuliwa
Mafanikio, yalirejesha utani wa kandanda la Ujerumani. Huku sasa ukifahamika kama “Der Klassiker”, michuano baina ya Borussia Dortmund na Bayern Munich ndiyo inayosuburuwa sana katika ratiba ya Bundesliga. Pamoja na uwezo wa Bayern kuwavutia mashabiki, ufufuo wa Jürgen Klopp wa BVB ulileta mpambano wa nafasi mbili za kwanza katika kandanda la Ujerumani
Kwaheri
Jürgen Klopp aliketi chini Jumatano, April 15, saa za mchana. Pamoja na mwenyekiti wa klabu Hans-Joachim Watzke na mkurugenzi wa michezo Michael Zorc. "ulikuwa uamuzi mgumu sana kwetu sote," alisema Watzke, kabla ya kumkumbatia. Klopp mwenye umri wa miaka 47 alikuwa katika hali yake ya ucheshi, akisema kuwa tayari ana tikiti tatu za msimu ujao. Klopp atakosekana sana katika Bundesliga msimu