JamiiGuinea-Bissau
Umeme warejeshwa Bissau baada ya serikali kulipa deni
19 Oktoba 2023Matangazo
Kampuni ya Kituruki ya Karpowership, imerejesha umeme katika mji mkuu wa Guinea-Bissau baada ya serikali kuanza tena kulipa deni la kampuni hiyo. Waziri wa uchumi wa Guinea-Bissau Suleimane Seidi aliwaambia waandishi wa habari jana Jumatano kwamba serikali imeweza kulipa kiasi cha dola milioni 6 kati ya 15 za malimbikizo ambazo inadaiwa.Kampuni hiyo ya Kituruki ilizima umeme katika taifa hilo la Afrika Magharibi kutokana na deni la dola milioni 17.
Guinea Bisau imekuwa ikitegemea kampuni hiyo ya umeme ya Uturuki kukidhi asilimia 100 ya mahitaji yake ya umeme tangu makubaliano yao ya mwaka 2019. Mnamo Septemba, kampuni hiyo ilizima usambazaji umeme katika mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown kutokana na deni la takriban dola milioni 40.