Umoja wa Afrika kupuuza waranti dhidi ya Gadaffi
3 Julai 2011Matangazo
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping amesema, Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague Uholanzi, inabagua. Mahakama hiyo inafuatiliza uhalifu uliotokea barani Afrika tu na hudharau uhalifu uliofanywa na nchi za Magharibi huko Iraq, Afghanistan au Pakistan.
Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amemtaka kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gadaffi kuondoka madarakani. Alitamka hayo, baada ya Gadaffi siku ya Ijumaa kuonya kuwa atashambulia miji ya Ulaya ili kulipiza kisasi operesheni ya NATO nchini Libya. Akiwa katika ziara rasmi nchini Uhispania, iliyo mshirika wa NATO, Clinton alisema, Gadaffi asaidie kuleta demokrasia badala ya kutoa vitisho.