Umoja wa Afrika unapigania viti viwili vya kudumu katika baraza la usalama
3 Julai 2005Umoja wa Afrika,unapigania viti viwili vya kudumu baraza la usalama litakapofanyiwa marekebisho.Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa mataifa 54 yanachama wamefikia msimamo huo wakati wa mkutano wao mjini Sirte nchini Libya.Mawaziri hao wa Umoja wa Afrika hawakuzitaja lakini nchi zenyewe zitakazouwakilisha umoja wa Afrika katika taasisi hiyo muhimu kabisa ya Umoja wa mataifa.Wanadiplomasia wanaamini nchi mbili kati ya sita; Afrika Kusini,Nigeria,Misri,Kenya,Libya na Senegal zina nafasi nzuri ya kuchaguliwa.Hadi sasa baraza la usalama la umoja wa mataifa lina wanachama watano tuu wa kudumu.Ujerumani,Japan,India na Brazil nazo pia zinapigania viti vya kudumu katika baraza la usalama.Nchi hizi nne zinataka pia Afrika ipatiwe viti viwili vya kudumu katika baraza la usalama.