Umoja wa Afrika warefusha vikwazo dhidi ya Nzuwani
29 Novemba 2007Matangazo
Moroni:
Umoja wa Afrika umerefusha kwa miezi miwili vikwazo dhidi ya kisiwa cha Komoro cha Nzuwani .Umoja wa Afrika umetoa mwito wakati huo huo wanajeshi wa kiafrika wanaopiga doria katika fukwe za visiwani hivyo vya bahari ya Hindi wazidishwe.Umoja wa Afrika umetangaza vikwazo vya usafiri dhidi ya kiongozi wa Nzuwani kanali Mohammed Bakar na maafisa wengine 140 wa kisiasa, na kijeshi wa kisiwa cha Nzuwani kwa kukataa kuitika mwito wa kuitisha uchaguzi huru kisiwani humo.Mali na miliki nyengine za viongozi hao zitaendelea kuzuwiliwa.Taarifa ya Umoja wa Afrika inatishia kuiwekea Nzuwani vikwazo vikali zaidi pindi madai ya kuitishwa uchaguzi huru hayataitikwa miezi miwili kutoka sasa.