Umoja wa Mataifa waahidi kubakia Afghanistan
6 Mei 2023Matangazo
Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kwamba ujumbe wa umoja huo nchini Afghanistan UNAMA, umeahidi kubakia nchini humo kwa niaba ya wanaume, wanawake na watoto wa Afghanistan.
Soma zaidi:Mataifa yajadili haki za wanawake wa Afghanistan
Umoja huo ulizindua tathmini iliyoangazia ikiwa itaendelea kufanya kazi na Taliban na hasa baada ya zuio hilo na hatimaye jana kutoa tamko hilo.
Katika taarifa iliyotolewa mjini Kabul, UNAMA ilirudia tena kulaani marufuku hiyo, ambayo imesema inadhoofisha majukumu yao na uwezo wa kufikia watu wote na kuahidi kuendelea kujadiliana na serikali namna watakavyoshirikiana.