UN yaitaka Urusi ikiri kukishambulia kijiji Ukraine
31 Oktoba 2023Wameitaka Urusi ifanye uchunguzi wa wazi kuhusu kilichotokea, itoe fidia kwa waathiriwa na iwawajibishe waliohusika.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Ufuatiliaji wa Haki za Binaadamu nchini Ukraine umesema katika ripoti iliyochapishwa leo kuwa ina ushahidi wa kutosha kuamini kuwa kombora la Urusi la masafa mafupi huenda lilisababisha mlipuko huo katika kijiji cha Hroza mnamo Oktoba 5.
Soma zaidi: Umoja wa Ulaya watofautina kuhusu msaada Ukraine
Shambulizi hilo lililopiga mgahawa mmoja kijiji hapo lilikuwa moja ya mashambulizi makali zaidi kuwahi kufanywa tangu vikosi vya Urusi vilianzisha uvamizi kamili nchini Ukraine miezi 20 iliyopita.
Familia zote ziliangamia wakati zikiwa katika hafla ya kumuaga askari wa eneo hilo aliyeuawa wakati akipigana na askari wa Urusi.
Mripuko huo uliwauwa wanawake 36, wanaume 22 na mvulana wa umri wa miaka minane.