Umoja wa Mataifa wajadili chuki dhidi ya Waislamu
11 Julai 2023Matangazo
Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk amesema matukio hayo yamefanywa kimakusudi ili kuchochea hasira na kuzigawanya jamii.
Ameongeza kuwa watu wanahitaji kuheshimu imani na tamaduni za wengine licha ya kuwa na misimamo tofauti.
Soma zaidi: Erdogan aonya Sweden kuhusu NATO baada ya kuchomwa Quran
Nakala ya kitabu cha Qur'an ilichomwa mbele ya msikiti katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm, mnamo Juni 28 na kuibua ukosoaji mkubwa kutoka mataifa ya Kiislamu.
Pakistan na mataifa mengine yamehimiza kufanyika majadiliano juu ya matukio yaliyopangwa ya chuki dhidi ya Uislamu katika baadhi ya mataifa ya Ulaya.