Wanawake wakulima wanakabiliwa na athari za kimazingira
5 Machi 2024Matangazo
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la chakula na kilimo duniani la FAO, iliyopewa kichwa cha habari "hali ya hewa isiyo ya haki", inaonyesha kuwa wanawake hao wanabaguliwa pindi wanapojaribu kutafuta vyanzo vingine vya mapato wakati wa majanga. Ripoti hiyo imebaini kwamba familia nyingi za vijijini zinazoendeshwa na mwanamke hupoteza kwa wastani asilimia 8 ya mapato yake wakati wa joto kali na asilimia 3 zaidi wakati wa mafuriko, ukilinganisha na familia zinazoongozwa na wanaume. FAO imeonya kwamba, ikiwa tofauti kubwazilizopo, katika uzalishaji wa kilimo na mishahara, baina ya wanaume na wanawake hazitoshughulikiwa, basi mabadiliko ya hali ya hewa yataongeza tofauti hizo katika miaka ijayo.