Umoja wa Mataifa wasema hali inazidi kuwa mbaya Libya
21 Agosti 2024Matangazo
Akitoa taarifa mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Stephanie Khoury amesema kuwa iwapo hakutokuwa na mazungumzo mapya ya kisiasa yatakayopelekea serikali itakayounganishwa na kufanyika kwa uchaguzi, nchi hiyo itashuhudia msukosuko mkubwa zaidi. Katika suala la uchumi, Khoury amesema kwamba majaribio ya kumbadilisha gavana wa Benki Kuu yanatokana na dhana za viongozi wa kisiasa na hata raia wa kawaida nchini Libya kwamba benki hiyo kuu inalifadhili eneo la mashariki tu na kulitelekeza eneo la magharibi. Libya ilitumbukia kwenye mapigano baada ya mapinduzi yaliyoongozwa na Jumuiya ya Kujihami ya NATO kumuondoa mamlakani Muamar Gadhafi.