Umoja wa Mataifa wasema Israel haizingatii ulinzi wa raia
19 Juni 2024Haya yalisemwa siku ya Jumatano (Juni 19) na Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Türk, mjini Geneva.
Türk alisema afisi yake imechunguza mashambulizi sita ya Israel katika Ukanda wa Gaza kati ya Oktoba 9 na Desemba 2.
Kauli ya mkuu huyo wa haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa ilitolewa, wakati kukiripotiwa mashambulizi ya angani ya Israel na mapigano kati ya vikosi vyake na wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza.
Soma zaidi:Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aikosoa Marekani kwa kuzuia silaha
Mashuhuda na mashirika ya ulinzi wa kiraia katika Ukanda wa Gaza yameripoti mashambulizi ya mabomu ya Israel magharibi mwa Rafah ambapo maafisa wa afya wanasema kuwa mashambulizi hayo yamewauwa watu saba.
Kwa upande mwengine, jeshi la Israel lilisema kwamba liko tayari kuwashambulia wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon kutoka kaskazini mwa Israel.