1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa watoa onyo kwa Rais Gbagbo.

Abdu Said Mtullya18 Desemba 2010

Shinikizo dhidi ya Laurent Gbagbo kuendelezwa.

https://p.dw.com/p/Qf8W
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemwonya Gbagbo dhidi ya kuzuia kazi za Umoja huo nchini Ivory Coast.Picha: AP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameionya serikali ya Ivory Coast dhidi ya kuuzuia Umoja wa Umoja wa Mataifa kufanya kazi zake nchini humo. Katibu Mkuu Ban amesema hali imegeuka kuwa ya hatari nchini Ivory Coast.

Amesema jaribio lolote la kuzuia kazi za Umoja wa Mataifa halitakubalika. Katibu mkuu huyo kwa mara nyingine amemtaka rais Laurent Gbagbo ajiuzulu na akubali kwamba kiongozi wa upinzani, Alassane Outtara ndiye alieshinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi uliopita na kuthibitishwa na Umoja wa Mataifa.

Hapo awali viongozi wa Umoja wa Ulaya walitishia kuweka vikwazo vya kiuchumi na wamempa rais Gbagbo muda wa hadi mwishoni wiki ili ajiuzulu.Habari zaidi zinasema jumuiya ya kimataifa inatayarisha vikwazo vya fedha ili kumlazimisha Gbago ajiuzulu.Wataalamu wamesema kuwa vikwazo hivyo vitaelekezwa katika akiba ya za benki.Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa bibi Michele Alliot-Marie amesema kuwa ni lazima kuendeleza shinikizo dhidi ya rais Gbagbo