1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Kofi Annan ahimiza makubaliano juu ya mageuzi kwenye Umoja wa mataifa

11 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEm8

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ameyataka mataifa wanachama kumaliza tofauti zao na kufikia makubaliano juu ya kufanyika mageuzi kwenye chombo hicho muhimu cha dunia ikiwa ni pamoja na kupanuliwa kwa baraza la usalama la Umoja huo.

Mapendekezo ya mageuzi hayo yatawasilishwa katika mkutano wa kilele wa viongozi wa dunia utakaofanyika mnamo septemba 14 hadi 16.

Mataifa wanachama wa umoja huo bado yanajaribu kutatua tofauti zilizopo juu ya mapendekezo nyeti ikiwa ni pamoja na kupanuliwa baraza la usalama,tafsiri ya ugaidi duniani,usimamizi wa bajeti,pamoja na mageuzi ya kiutawala katika chombo hicho miongoni mwa mengine.

Hata hivyo inaonyesha kwamba matumaini ya kufikia maridhiano yatakayowezesha kuongezwa kwa wanachama wapya kwenye baraza la usalama la umoja huo yamefifia.