Umoja wa Ulaya kulazimika kuiongezea msaada Ukraine
16 Februari 2024Taasisi ya Utafiti ya Kiel inayofuatilia masuala ya msaada yenye makao yake nchini Ujerumani ilisema katika ripoti yake kuhusu hali ya msaada wa kijeshi, kifedha na kibinaadamu kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi wa Februari 24, 2022, kuwa haijulikani ikiwa Marekani itatuma msaada zaidi wa kijeshi mwaka huu wa 2024.
Soma zaidi: Stoltenberg aonya dhidi ya kuigawa Marekani na Ulaya
Kulingana na takwimu zake za hadi Januari 15, 2024, Marekani ilikuwa imetuma dola bilioni 45.4 za msaada wa kijeshi kwa Ukraine kati ya Februari 2022 na Desemba 2023, ikiwa ni karibu na euro bilioni mbili kwa mwezi.
Umoja wa Ulaya na wanachama wake 27 umeahidi msaada wa kijeshi wa euro bilioni 49.7 tangu kuanza kwa vita, lakini kufikia sasa umetoa au kutenga euro bilioni 35.2 tu.