1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya mtandaoni yaliyofanywa na Urusi yakosolewa

3 Mei 2024

Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO wametoa taarifa ya kulaani shambulizi la mtandaoni lililofanywa na Urusi nchini Ujerumani ambalo pia Jamhuri ya Czech inasema ililengwa.

https://p.dw.com/p/4fUZC
EU Brüssel Josep Borrel
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel Picha: Dursun Aydemir/Andalou/picture alliance

Taarifa ya Umoja wa Ulaya iliyotolewa na Mkuu wa Sera za Kigeni Josep Borrel imesema umoja huo wenye wanachama 27 umedhamiria kuchukua hatua kamili za kuzuia na kujibu tabia hiyo mbaya ya Urusi mitandaoni.

Amesema, wanalaani vikali uhalifu huo wa mitandaoni wenye nia ya kudhoofisha taasisi zao za kidemokrasia, usalama wa taifa na jamii huru.

Yenyewe Urusi imekanusha vikali kuhusika kwa namna yoyote na tuhuma hizo.