Umoja wa Ulaya unasema uko tayari kusaidia juhudi za amani za umoja wa Afrika katika jimbo la Darfour
24 Mei 2005Matangazo
Umoja wa Ulaya uko tayari kusaidia juhudi za amani za umoja wa Afrika katika jimbo la magharibi la Sudan Darfour.Habari hizo zimetangazwa baada ya mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa umoja wa ulaya mjini Brussels.Misaada ya Umoja wa ulaya itahusiana zaidi na shughuli za usafiri wa nchi kavu na angani.Zaidi kuhusu misaada hiyo itafafanuliwa katika mkutanao wa wafadhili alkhamisi ijayo mjini Addis Ababa.