1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU kushirikiana kiusalama na ulinzi na Japan, Korea Kusini

23 Juni 2024

Umoja wa Ulaya unatafuta ushirikiano wa sekta ya usalama na ulinzi na Japan na Korea Kusini kwa lengo la maendeleo ya pamoja ya vifaa vya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4hPIc
Future Combat Air System (FCAS)
Programu ya muundo wa mifumo ya ndege ya teknolojia mpya. Picha: Peter Byrne/empics/picture alliance

Taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la Nikkei, likimnukuu afisa mwandamizi wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya.

Jarida hilo lenye kujikita katika habari za biashara la Japan limesema hatua hiyo itakuwa kubwa ya kwanza ya aina yake kwa Umoja wa Ulaya katika ushirikiano wa kiusalama na ulinzi.

Umoja huo unatarajia kufikia makubaliano ya ngazi ya mawaziri na Japan ifikapo mwisho wa mwaka, ambayo inaweza kusaidia Umoja wa Ulaya kufadhili miradi ya pamoja ambayo itasimamiwa na makampuni ya Kijapani na Ulaya.

Hata hivyo, wawakilishi wa wizara za mambo ya nje za Japan na Korea Kusinipamojana ujumbe wa Umoja wa Ulaya huko Tokyo haukuweza kupatikana mara moja ili kuweza kutoa kauli yao kufuatia taarifa hiyo.