EU iko tayari kuzungumza na Marekani kuhusu China
21 Januari 2025Tangazo la kiongozi huyo wa juu wa Umoja wa Ulaya amelitowa katika Jukwaa la kiuchumi duniani, huko Davos,Uswisi, huku Beijing ikionya dhidi ya kuanzishwa vita vibaya vya kibiashara kutokana na sera ya rais Donald Trump ya kulinda biashara za Marekani dhidi ya ushindani.
China na Marekani zinaweza kufikia mangi zikiungana na kufanya kazi pamoja
Pamoja na kwamba Trump hayuko kwenye mkutano huo wa Kimataifa,ajenda kubwa huko Davos kwa viongozi wa makampuni na wa kisiasa ni kurejea kwa kiongozi huyo katika ikulu ya Marekani.
Umoja wa Ulaya na China inayowakilishwa kwenye mkutano huo na naibu waziri mkuu wake Ding Xuexiang, wamesema sera ya kuzilinda biashara dhidi ya ushindani haiwezi kufika kokote na hakuna washindi katika vita vya kibiashara.