UN: Jamhuri ya Afrika ya Kati yaathirika na mzozo wa Sudan
15 Juni 2024Katika ripoti iliotolewa na kamati ya wataalamu ilioundwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ilioonesha wasiwasi kuhusu "athari za ziada" katika mzozo huo inasema kwamba, Jamhuri ya Afrika ya Kati imeathirika pakubwa na mzozo unaoendelea Sudan.
Ripoti ya kamati hiyo iliangalia masuala kadhaa ikiwemo hali ya kiutu wakati taifa hilo likishuhudia wimbi la mamilioni ya wakimbizi kutoka Sudan, uvamizi wa pande mbili zinazohasimiana pamoja na uvamizi wa anga wa jeshi la Sudan karibu na kituo cha mpakani cha Umm Dafog ambapo ni kitovu cha wanamgambo wa RSF.
Soma pia:Marekani yaongeza msaada kwa Sudan kupambana na njaa
Aidha wataalamu hao wa Umoja wa Mataifa wameitolea mwito serikali ya Afrika ya Kati kukabiliana na ongezeko la biashara haramu ya silaha kutoka mataifa jirani ikizingatiwa hali ilivyo kwa sasa nchini Sudan.