SiasaAsia
UN: Korea Kaskazini yazidisha ukandamizaji, watu wafa njaa
18 Agosti 2023Matangazo
Kuna pia ripoti za watu kufa kwa njaa katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo, huku hali ya uchumi ikizidi kuwa mbaya.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa ofisi ya Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk katika mkutano wa kwanza wa haki za binaadamu kuhusu Korea Kaskazini tangu mwaka 2017.
Kiongozi huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa amesema taarifa walizonazo ni kwamba watu wamekuwa na hofu ya kufuatiliwa na serikali, kukamatwa, kuhojiwa na kuwekwa kizuizini.
Kama mifano ya kuongezeka kwa ukandamizaji wa haki za binadamu, alisema, mtu yeyote anayepatikana na hatia ya kufuatilia habari za itikadi za kigeni na haswa kutoka Korea Kusini inawezekana akafungwa miaka 5 hadi 15 gerezani.