UN: Kuna uwezekano wa uhalifu dhidi ya ubinaadamu Libya
5 Oktoba 2021Wachunguzi hao waliopewa jukumu la kufuatilia hali ya taifa hilo la kaskazini mwa Afrika na Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa, walisema kwenye taarifa yao ya jana kwamba uhalifu huo ulifanyika dhidi ya raia na wahamiaji waliokamatwa wakijaribu kwenda Ulaya.
Taarifa hiyo ilitolewa wakati kukiwa pia na ripoti ya msako usiotegemewa nchini Libya, ambao umepelekea kukamatwa kwa wahamiaji zaidi ya 5,000, wakiwemo mamia ya wanawake na watoto.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ghasia zilizosababishwa na msako huo zilipelekea kifo cha mtu mmoja.
Serikali ya Libya haijasema kitu kuhusu ugunduzi huo wa Umoja wa Mataifa, ingawa ilisema msako wa wahamiaji ulikuwa sehemu ya operesheni za usalama dhidi ya wahamiaji haramu na wauzaji madawa ya kulevya.