1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN, mashirika ya haki wasifu hatua ya Cameroon kukiri makosa

23 Aprili 2020

Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu wamsema hatua ya serikali ya Cameroon kukiri kwamba wanajeshi wake walishiriki katika mauaji ya raia mwezi Februari ni hatua chanya.

https://p.dw.com/p/3bKJ1
Kamerun Symbolbild Soldaten im Norden ARCHIV
Picha: Getty Images/AFP/R. Kaze

Awali serikali ilikanusha ushiriki katika umuagaji huo wa damu katika mkowa wa Northwest, ambako wazungumzaji Kiingereza wanaotaka kujitenga wamekuwa wakipambana dhidi ya vikosi vya serikli kwa miaka miwili iliyopita.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vifo vilivyotokana na mapigano ya usiku wa Februari 13 hadi 14, vilikuwa vya raia 23, wakiwemo watoto 15 katik kijiji cha Ngarbuh.

Umoja wa Mataifa ulisema watoto tisa walikuwa chini ya umri wa miaka mitano, na kwamba wawili kati ya wahanga walikuwa wanawake wajawazito.

Ofisi ya rais ilisema katika taarifa siku ya Jumanne, kwamba wanajeshi watatu na kundi la walinzi wa vijiji walivamia kambi ya waasi na kuuwa watano, kabla ya kugundua kwamba wanawake watatu na watoto 10 waliuawa katika mripuko wa chombo kilichokuwa na mafuta ndani yake.