UN: Mzozo nchini Sudan unazidi kuwa mbaya zaidi
18 Januari 2025Kamishna wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema mzozo wa kivita unaoendelea nchini Sudan unazidi kuwa mbaya zaidi kwa raia.
Turk ameelezea ripoti zinazoonyesha kwamba makumi ya watu wameuawa katika mashambulizi ya kikabila yaliyolengwa katika jimbo la kusini-mashariki la al-Jazirah na mji mkuu wa Khartoum ambapo vikosi vya kijeshi vya serikali na wanamgambo wa RSF vinapambana kuchukua udhibiti.
Soma zaidi. Marekani yaandaa mazungumzo ya kusitisha mapigano Sudan
Mapigano kati ya Wanajeshi wa Sudan (SAF), wakiongozwa na Jenerali Abdel-Fattah al-Burhan, na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), vilivyo chini ya Mohamed Hamdan Daglo, yameongezeka kwa kiasi kikubwa katika wiki za hivi karibuni. Türk amesema.
Tayari Marekani imewaweka vikwazo kwa al-Burhan na Daglo.Umoja wa mataifa unasema mzozo wa Sudan wa tangu April 2023 umesababisha karibu watu milioni 12 kuyakimbia makazi yao na kuwafanya mamilioni kwa wakimbizi.