UN: Ulimwengu unarudi nyuma kutimiza malengo ya mazingira
9 Septemba 2023Tathmini ya miaka miwili ya malengo ya makubaliano ya mazingira ya Paris ya mwaka 2015 imegundua kuwa juhudi za ulimwengu kuyanusuru mazingira zinapungua kwa kiasi kikubwa.
Katika ripoti iliyotolewa jana, Umoja wa Mataifa umesema kuwa ulimwengu uko nje ya lengo lililokusudiwa la kupunguza ongezeko la joto duniani, na kutoa wito wa hatua zaidi za kukomesha matumizi ya nishati ya mafuta na kufikia malengo ya makubaliano ya Paris.
Aidha, Umoja wa Mataifa umeonya kwamba ahadi zilizopo za kupunguza hewa chafu zinazosababishwa na uchomaji wa nishati ya mafuta hazitoshi kukabiliana na ongezeko la joto duniani.Guterres:Tuchukue hatua za pamoja ama tuangamie sote
Mataifa mengi ya Kiafrika, ambayo tayari yamezama katika lindi la madeni, yanajitahidi kujiondoa kutoka kwenye nishati ya visukuku wakati zikikabiliwa na athari za ukame unaozidi kuwa mbaya, mafuriko, joto kali na vimbunga.