1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Vijana wanakabiliwa na wimbi la ukatili

10 Oktoba 2024

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya watoto ameonya kwamba vijana wanakabiliwa na wimbi la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ambao haujawahi kushuhudiwa.

https://p.dw.com/p/4lcR6
Sudan Konflikt Gadaref
Picha: AFP

Ukatili huo unasababishwa na vita, mabadiliko ya hali ya hewa, njaa pamoja na uhamishwaji.

Najat Maalla M'jid, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili dhidi ya Watoto amesema  watoto hawahusiki na vita, wala migogoro lakini wanapitia changamoto.

Hii leo M'jid, atawasilisha ripoti yake katika mkutano wa Umoja wa Mataifa inayoonyesha ukatili dhidi ya watoto umeenea, na kwamba teknolojia inawezesha uhalifu dhidi ya vijana kuliko hapo awali.

Ripoti hiyo inaonyesha kwamba zaidi ya watoto milioni 450 waliishi katika maeneo yenye migogoro kufikia mwishoni mwa 2022, asilimia 40 ya watu milioni 120 waliokimbia makazi yao mwishoni mwa Aprili walikuwa watoto, na watoto milioni 333 wanaishi katika umaskini uliokithiri.