UN: Wanawake na watoto waliuwawa zaidi Afghanistan
26 Julai 2021Hii ni idadi kubwa kuliko miezi sita ya mwaka wowote tangu Umoja wa Mataifa ulipoanza utaratibu huu wa kuweka hesabu za vifo mwaka 2009.
Ripoti hiyo imenakili ongezeko la asilimia 47 la raia waliouwawa na kujeruhiwa katika vurugu miezi sita ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana. Soma Taliban wakamata eneo kubwa la Afghanistan
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Deborah Lyons, amewasihi viongozi wa Taliban na Afghanistan wazingatie upya njia mbaya na za kutisha zinazoambatana na athari ya mzozo huo kwa raia.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan umeripoti raia 1,659 waliuawa na 3,254 walijeruhiwa. Huku wanawake na watoto wakifikia karibu nusu ya raia wote waliouwawa. Soma UNHCR yahofia kwamba Waafghanistan zaidi wataikimbia nchi yao
Watoto, 468 waliuawa na wengine 1,214 walijeruhiwa na wanawake 219 waliuawa na 508 walijeruhiwa.
Mauwaji na majeruhi waongezeka
Ripoti hiyo imegundua ongezeko kubwa la mauaji na majeruhi tangu Mei, wakati vikosi vya majeshi ya kimataifa vilipoanza kuondoka na mapigano yalizidi kutoka kwa Taliban. Soma zaidi Dola Milioni 100 kuwasaidia wakimbizi wa Afghanistan
Mkuu wa haki za binadamu wa Ujumbe wa Usaidizi wa Umoja wa Mataifa (UNAMA) nchini Afghanistan Fiona Frazer amesema "Shambulio baya zaidi kutokea, lilifanyika Mei 8, karibu na shule ya Kabul ambapo zaidi ya raia 300 walipata majeraha ya mabomu yaliyotegwa ardhinio matatu, wengi wao walikuwa wasichana wa shule ambao walikuwa wakiondoka kwenda nyumbani siku hiyo."
Taliban limeyateka maeneo muhimu katika wiki za hivi karibuni, huku kundi hilo likiteka pia eneo la kimkakati la mpaka na sasa linatishia kuteka miji mikuu kadhaa nchini Afghanistan.
Kipi wanachotaka Taliban?
Wakati wanachukua maeneo makubwa, Kundi la Taliban limesema halitaki kuhodhi madaraka lakini, wanasisitiza hakutakuwa na amani nchini Afghanistan mpaka kuwe na mazungumzo mapya na serikali ya Kabul na Rais Ashraf Ghani kuondolewa madarakani. Soma zaidi Kufikia amani, Taliban yataka rais wa Afghanistan kuondoka
Lyons, mjumbe wa Umoja wa Mataifa ambaye pia anaongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa Afghanistan, amewataka viongozi wa Taliban na Afghanistan wazidishe juhudi zao kwenye meza ya mazungumzo ili kulinda watu wa taifa hilo na kuwapa matumaini ya maisha bora ya baadaye.
Chanzo//AFP