SiasaSudan
UN: Washirika wanaopeana silaha Sudan walaumiwa
13 Novemba 2024Matangazo
DiCarlo aliliambia Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa kwamba mapigano hayo yanatakiwa yasimamishwe mara moja.
Amesema vikosi hivyo vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 24,000 na pia vimesasbabisha mzozo mbaya zaidi duniani wa watu kulazimika kuyahama makazi yao kwa ajili ya kukimbia vita amesisitiza kwamba matukio hayo hayakubaliki na yanakiuka sheria.
Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo ametoa wito wa kuzilazimisha pande zinazopigana nchini Sudan zikubali kufanya mazungumzo.
Hivi majuzi Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kuwa nchi hiyo iko ukingoni kutmbukia kwenye baa la njaa.