MigogoroMamlaka ya Palestina
Watu 576,000 ukingoni mwa kutumbukia kwenye baa la njaa Gaza
28 Februari 2024Matangazo
Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Ramesh Rajasingham amesema mtoto mmoja kati ya sita walio chini ya umri wa miaka miwili kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, anakabiliwa na utapiamlo.
Mkuu huyo ameongeza kuwa, watu wote milioni 2.3 katika ukanda huo wa Gaza wanategemea misaada ya chakula ili kuendelea kuishi.
Soma pia: Israel yatishia kushambulia Rafah wakati wa Ramadhan
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Carl Skau ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, shirika hilo liko tayari kupeleka misaada ya kibinadamu kwa wahitaji huko Gaza iwapo kutakuwepo na makubaliano ya kusitisha mapigano.