JamiiUturuki
UN yachangisha robo ya fedha za msaada kwa Uturuki
31 Machi 2023Matangazo
Kulingana na msemaji wa shirika la misaada ya kiutu la Umoja wa Mataifa, Jens Laerke aliyekuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, kufikia sasa wafadhili wamechangisha dola milioni 268 kati ya dola bilioni moja zinazotakiwa.
Marekani, Kuwait, Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa, CERF na Saudi Arabia kwa sasa ndio waliochangisha kiasi kikubwa cha fedha kufikia sasa.
Laerke anasema Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada wamefanikiwa kuwasaidia zaidi ya watu mioni 4.1.