1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaitaka Iran kufuta sheria mpya kali ya hijab

22 Septemba 2023

Umoja wa Mataifa umeitolewa wito Iran kufuta sheria mpya inayoogeza adhabu kwa wanawake wanaokiuka kanuni ya uvaaji, ikiielezea kama kandamizi na kutweza.

https://p.dw.com/p/4WhcL
Iran |
Binti wa Iran akihudhuria mkutano unaounga mkono vazi la HijabPicha: Atta Kenare/AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa umeitolewa wito Iran kufuta sheria mpya inayoogeza adhabu kwa wanawake wanaokiuka kanuni ya uvaaji, ikiielezea kama kandamizi na kutweza.

Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema imehuzunishwa pakubwa na upitishaji wa kile kinachoitwa muswada wa Usahili na Hijabu, unaotishia wanawake wa Kiiran wasiovaa mavazi ya stara kwa kifungo cha hadi miaka 10 gerezani.

Mbali ya vifungo virefu na faini kubwa, chini ya sheria hiyo, wale wanaokutwa na hatia ya ukiukaji wanaweza pia kuchapwa viboko na kukabiliana na vikwazo vya kusafiri.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Turk, amesisitiza kuwa sheria hiyo kandamizi inakiuka sheria ya kimataifa, na kwamba inapaswa kufutiliwa mbali.