1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yalaani mashambulizi dhidi ya ujumbe wake Lebanon

Sylvia Mwehozi
14 Novemba 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya wiki za hivi karibuni dhidi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon unaofahamika kwa kifupi kama UNIFIL.

https://p.dw.com/p/4mxYf
UNIFIL Lebanon
Ujumbe wa UNIFIL-LebanonPicha: picture alliance/dpa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi ya wiki za hivi karibuni dhidi ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon unaofahamika kwa kifupi kama UNIFIL.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano, Baraza la Usalama limezitolea mwito pande zote kuheshimu ulinzi na usalama wa maafisa wa kikosi hicho na maeneo yake. 

Soma: Israel yashambulia makao makuu ya UN Lebanon

Taarifa hiyo imeongeza kwa kusema kuwa walinda amani wote hawapaswi kulengwa katika mashambulizi ya aina yoyote, ikitaja haswa mashambulizi ya Oktoba 29, Novemba 7 na 8.

Hivi karibuni ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, ulilituhumu jeshi la Israel kuwa lilifanya uharibifu wa kudhamiria wa mali na miundombinu yake.