1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN yaonya juu ya janga kubwa kanda ya Mashariki ya Kati

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon, Jeanine Hennis-Plasschaert, ameonya kuwa eneo la Mashariki ya Kati linakabiliwa na hali mbaya.

https://p.dw.com/p/4kx3Q
Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon, Jeanine Hennis-Plasschaert
Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon, Jeanine Hennis-Plasschaert Picha: Hadi Mizban/AP Photo/picture alliance

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon, Jeanine Hennis-Plasschaert, ameonya kuwa eneo la Mashariki ya Kati linakabiliwa na hali mbaya na kuongeza kuwa kanda hiyo ipo ukingoni mwa janga kubwa linalonyemelea. Mratibu huyo amesisitiza kwamba hakuna suluhisho la kijeshi ambalo litafanya pande mbili kuwa salama.

Matamshi ya mratibu huyo yanarejelea makabiliano makali yanayoendelea kati ya jeshi la Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah nchini Lebanon usiku kucha kuamkia Jumapili. Pande zote mbili zimeshambuliana vikali tangu makabiliano mapya yalipozuka karibu mwaka mmoja uliopita.

Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Mataifa UNIFIL umekuwa ukifuatilia mpaka wa Israel na Lebanon tangu mwaka 1978. Mwezi uliopita, wanajeshi watatu wa UNIFIL walijeruhiwa kidogo na mlipuko uliotokea karibu na gari lao kusini mwa Lebanon.