UN: Taliban wawakosesha kazi watu 3,300 wakiwemo wanawake.
7 Aprili 2023Umoja wa Mataifa umesema wafanyakazi wake 3,330 wa Afghanistan wanaowajumuisha wanaume na wanawake, jana walibaki majumbani kwa siku ya pili kupinga marufuku ya Taliban dhidi ya wafanyakazi wanawake wa Umoja huo wanaofanya kazi nchini humo huku ukiendelea kushinikiza uamuzi huo ubatilishwe. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, limefanya mkutano wa dharura kuhusu hatua hiyo ya Taliban na kushinikiza wito wake wa marufuku hiyo kubatilishwa. Msemaji wa Umoja huo, Stephane Dujarric, amesisitiza wito huo wa Umoja wa Mataifa kwamba wafanyakazi wake wote wanahitaji kuwasilisha msaada wa kuokoa maisha kwa mamilioni ya watu nchi humo na kusisitiza tena kwamba wanawake wa Afghanistan hawatabadilishwa na wanaume. Dujarric pia amesema kuwa Umoja wa Mataifa hautaki kujipata katika hali ambayo inawabadilisha wanawake wa Afghanistan na wanawake kutoka nje ya nchi hiyo ambao hawajapigwa marufuku kufanya kazi nchini humo.