UN yasema watoto 7 wamekufa kwa baridi kali huko Gaza
6 Januari 2025Matangazo
Kupitia mtandao wa X, Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limesema kwamba watoto wachanga 7,700 katika eneo hilo lenye vita wanaishi katika makazi duni kutokana na mgogoro kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas. Mamlaka ya Israel inayohusika na masuala ya Palestina, COGAT,imesema kwenye mtandao wa X kwamba inafanya kazi na mashirika ya misaada ya kimataifa kama vile shirika la Rahma Worldwide ili kuwapa wakazi mahema, blanketi,nguo za joto na bidhaa za usafi.