UN yastushwa na sheria ya maadili ya Afghanistan
25 Agosti 2024Mnamo Jumatano, serikali ya Afghanistan ilitangaza uanzishaji wa sheria yenye vifungu 35 inayoelezea kwa kina miongozo ya tabia na mtindo wa maisha vinavyozingatia tafsiri yake ya Sheria ya Kiislamu.
Sheria hiyo inaweka adhabu za hatua kwa hatua za ukiukaji, kuanzia maonyo ya madomo hadi vitisho, faini na vifungo vya urefu tofauti, zinazotekelezwa na polisi wa maadili waliyoko chini ya Wizara ya Uenezaji wa Maadili na Kuzuwia Maovu.
Soma pia:Taliban yamzuia mtaalamu wa UN kuingia Afghanistan
Mkuu wa Ujumbe wa Msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA, Roza Otunayeva, amesema ni maono yanayotatiza kwa Afghanistan, ambapo wakaguzi wa maadili wana mamlaka ya hiari kutisha, na kumuweka kizuwizini mtu yeyote kwa msingi wa orodha ndefu ya ukiukaji, ambayo wakati mwingine haiko wazi.