Kuna mijadala kuwa kizazi cha sasa cha vijana maarufu kama "millennials" kinapendelea zaidi hela kama kigezo muhimu kuzama katika bahari ya mapenzi. Wanaume walikuwa wanatumia muda mwingi kufanya mazoezi ya viungo ili kuonyesha misuli yao na kutaka kuvutia zaidi mbele ya wasichana. Je, mabinti wanapendelea misuli au utajiri wa mwanaume wakati linapokuja suala la kuanzisha mahusiano ya kimapenzi?