UN:Bajeti ya 2020 juu, fedha za uchunguzi uhalifu wa kivita
28 Desemba 2019Bajeti hiyo inawakilisha ongezeko dogo kutoka idadi ya mwaka 2019 ya dola bilioni 2.9. Ongezeko hilo ni kutokana na ujumbe wa ziada unaliowekwa katika sekretariati ya Umoja wa mataifa , ughali wa maisha na marekebisho ya kiwango cha ubadilishaji fedha, kwa mujibu wa wanadiplomasia.
Hizi ni pamoja na ujumbe wa uangalizi nchini Yemen , ujumbe wa kisiasa ulioundwa nchini Haiti, uchunguzi wa uhalifu wa kivita uliofanyika nchini Syria tangu kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011, na Myanmar baada ya ukandamizaji wa mwaka 2017 dhidi ya waislamu Warohingya ambao ni jamii ya wachache nchini humo.
Kwa mara ya kwanza , bajeti kwa ajili ya uchunguzi nchini Syria na Myanmar, ambao hapo awali ulikuwa ukigharamiwa na michango ya hiari, katika mwaka 2020 utahamishiwa katika bajeti ya sekretariati ya Umoja wa mataifa na utapatiwa michango ya lazima kutoka kwa matifa wanachama 193.
Urusi ilipendekeza mabadiliko kadhaa wakati wa majadiliano katika kamati juu ya mikutano ya masuala ya bajeti na kikao cha utendaji cha baraza kuu la Umoja wa mataifa.
Maazimio ya UN
Katika kila kura , Urusi, Syria, Myanmar na waungaji mkono wao, ikiwa ni pamoja na Korea kaskazini, Iran, Nicaragua na Venezuela, kulikuwa na wingi mkubwa dhidi yao. Wote wamesema kuwa wanajitenga na maelezo ya mfumo wa uchunguzi katika maazimio hayo yaliyoidhinishwa.
Urusi imesema itachunguza malipo yake ya lazima ya hapo baadaye kutokana na matokeo ya kura na kutabiri ongezeko la malipo ya nyuma ambayo kwa hivi sasa yanakabili hazina ya Umoja wa mataifa kutokana na mataifa kutolipa vya kutosha.
Urusi imedai jana Ijumaa kuwa mfumo wa uchunguzi hauna uhalali, wakati Syria imesisitiza kuwa haina mamlaka kutoka baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.
Bajeti ya matumizi ya Umoja wa mataifa ni tofauti kutoka bajeti ya mwaka kwa ajili ya operesheni za kulinda amani ya kiasi cha dola bilioni 6 ambazo ziliidhinishwa mwezi Juni.