1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UNHCR yatoa wito kwa Ujerumani kuipa ufadhili zaidi

20 Januari 2024

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi, ametoa wito kwa Ujerumani na mataifa mengine kulifadhili shirika hilo katikati ya ongezeko la mahitaji ya kibinadamu.

https://p.dw.com/p/4bUby
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi.
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi.Picha: Noam Galai/Getty Images/AFP

Filippo Grandi amesema anatumai kuwa Ujerumani haina nia ya kupunguza ufadhili wake ndani ya shirika hilo licha ya nchi hiyo kukabiliwa na mzozo kwenye bajeti yake.

Ujerumani ni nchi ya tatu inayotoa ufadhili mkubwa katika shirika hilo la kushughulikia wakimbizi baada ya Marekani na Umoja wa Ulaya.

Hivi karibuni, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu imeshuhudia hitaji la kuwepo kwa ufadhili zaidi kutokana na kuongezeka kwa mizozo duniani na kuongezeka kwa mfumuko wa bei.

Grandi ametahadharisha juu ya athari ambazo zinaweza kujitokeza iwapo shirika hilo litapunguziwa ufadhili ikiwemo ongezeko la mzozo wa uhamiaji.