Union Berlin kumkabili Kruse ugenini Wolfsburg
3 Machi 2022Kocha wa klabu ya Union Berlin Urs Fischer amekataa kusema lolote kuhusu kumkabili mshambuliaji wa zamani wa timu yake Max Kruse katika mechi ya Bundesliga ugenini Wolfsburg Jumamosi.
"Nafikiri yamezungumzwa ya kutosha kuhusu suala hili. Sitalizungumzia. Muhimu ni kukubali changamoto ya Wolfsburg na Max ni sehemu ya mchezo wao," Fischer aliwaambia waandishi habari Alhamisi.
Katika hatua ya kushangaza, Kruse aliondoka Union kuhamia Wolfsburg mwezi Januari mwaka huu, bila kuficha kwamba alikuwa atapata fedha nyingi huko na pia kuonesha ukosoaji wa miezi yake ya mwisho Berlin.
Union ilipoteza mechi tatu bila kufunga bao baada ya Kruse kuondoka lakini hatimaye wakarejea katika fomu yao katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Mainz wikendi iliyopita na siku ya Jumanne wakafanikiwa kufuzu kwa nusu fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani kwa kuwazidi nguvu St Pauli Hamburg 2-1.
Union wamesema hakuna kipengee katika mkataba wa Kruse ambacho kingemzuia kucheza dhidi yao, huku msemaji wa klabu hiyo, Christian Arbert, akisema usimamizi wa klabu haujapoteza hata fikra kusisitiza juu ya kifungu kama hicho.
(dpa)