SiasaAfrika Kusini
Upinzani Afrika Kusini wataka kusitishwa uhusiano na Israel
18 Oktoba 2024Matangazo
Malema amemhoji Rais Ramaphosa katika kipindi cha maswali na majibu bungeni kisha akamtaka spika wa bunge hilo Thoko Didiza kuweka shinikizo kwa Rais ili aweze kutimiza ahadi aliyoitoa mwaka jana ya kuufunga ubalozi wake nchini Israel.
Akijibu hoja ya Julius Malema Bungeni, Rais Cyril Ramaphosa amesema bado anafikiria kusitisha uhusiano wote wa kidiplomasia na Israel na kwamba msimamo wa serikali kuhusu Israel haujabadilika na uungaji mkono kwa Palestina hauwezi kubatilishwa.
Mwaka jana Bunge la Afrika Kusini lilipiga kura ya kuufunga ubalozi wa Israel mjini Pretoria ikiwa ni pamoja na kuishinikiza serikali ikate kwa muda uhusiano wa kidiplomasia na Israel hadi makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza yatakapoafikiwa.