Upinzani Bangladesh waitisha mgomo wa nchi nzima Jumapili
28 Oktoba 2023Maandamano ya leo yalisambaratika kufuatia makabaliano makali baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama. Polisi mmoja amekufa na wengine kadhaa wamejeruhiwa kwenye mapambano yaliyotokea kati
kati mwa mji mkuu wa nchi hiyo Dhaka pale wafuasi wa upinzani walipoitikia wito wa kuandamana kumshinikiza Waziri Mkuu Sheikh Hasina kuachia madaraka kuelekea uchaguzi unaokuja.
Soma zaidi: Maelfu waandamana Bangladesh kumtaka Waziri Mkuu kujiuzulu
Katibu Mkuu wa chama cha Bangladesh Nationalist (BNP), ametoa mwito wa mgomo wa nchi nzima kesho ikiwa ni mwendelezo la shinikizo kwa Bibi Hasina aridhie kujiuzulu kupisha maandalizi ya uchaguzi.
Upinzani unataka kuundwe serikali ya mpito isiyoegemea upande wowote wa vyama itakayokuwa na dhima ya kusimamia uchaguzi unaokuja wa mnamo mwezi Januari ili kuufanya uwe huru na wa haki.