Upinzani DRC wazungumzia kupendelewa muungano tawala
20 Februari 2023Matangazo
Zaidi ya wapiga kura milioni 50 wa Kongo wanatakiwa kuandikishwa ifikapo Machi 17, lakini Tume ya Uchaguzi, CENI, siku ya Ijumaa ilisema idadi isiyojulikana na vituo vya kuandikishia katika majimbo 10 havikufikia muda wa mwisho uliowekwa, ambao tayari umeongezwa kwa siku 25.
Mgombea wa upinzani, Martin Fayulu, amesema kuna vituo vilivyopo katika orodha ya tume ambavyo havijafunguliwa na vingine ambavyo vimefunguliwa ingawa havikupaswa kuwa wazi.
Fayulu amesema kuna matatizo mengi ikiwemo vyanzo vya umeme kwenye mashine na ucheleweshaji wa vifaa.
Mgombea mwingine, Moise Katumbi amesema anaamini kuwa CENI ilikuwa inatoa kipaumbele katika kuwaandikisha waiga kura kwenye maeneo yanayomuunga mkono Rais Felix Tshisekedi, likiwemo jimbo la Kasai.