1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Upinzani Korea Kusini utajaribu tena kumtoa Yoon madarakani

8 Desemba 2024

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Korea Kusini Lee Jae-myung, amesema chama hicho kitajaribu tena Desemba 14 kumuondoa madarakani rais Yoon Suk Yeol, kufuatia hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi.

https://p.dw.com/p/4nt20
Korea Kusini | Lee Jae-myung
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Korea Kusini Lee Jae-myungPicha: Yonhap/REUTERS

Akizungumza na waandishi habari Lee amesema Yoon aliyemtaja kama muasi na anayejaribu kuvuruga utaratibu wa katiba anapaswa kujiuzulu mara moja au aondolewe kwa nguvu madarakani. 

Wakati huo huo polisi imemtia nguvuni waziri wa ulinzi anayehusika na masuala ya operesheni ya sheria ya kijeshi huku waziri wa ndani akijiuzulu. Wote kwa sasa wanachunguzwa kwa madai ya uasi. 

Rais wa Korea Kusini aomba radhi kwa taifa

Maelfu ya raia wa Korea Kusini wanaendelea kuandamana wakimtaka rais Yoon kuondoka madarakani.