1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTogo

Upinzani nchini Togo wawataka wengi kujitokeza kupiga kura

26 Aprili 2024

Vuguvugu la upinzani nchini Togo jana Alhamisi ulitoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa bunge utakaofanyika Aprili 29 na ambao umegubikwa na mjadala juu ya mageuzi ya kikatiba.

https://p.dw.com/p/4fCSw
Rais wa Togo Faure Gnassingbé
Upinzani nchini Togo unapinga mageuzi ya kikatiba wakidai yanalenga kumbakisha Rais Faure Gnassingbe(pichani) kubakia madarakani milele Picha: Filip Singer/EPA Pool/dpa/picture alliance

Wasiwasi wa kisiasa umeongezeka nchini Togo tangu wabunge walipoidhinisha mwezi huu mageuzi ambayo upinzani unaamini yatamruhusu Rais Faure Gnassingbe, kuongeza muda wake madarakani.

Gnassingbe alimpokea baba yake aliyelitawala taifa hilo dogo la Afrika ya Magharibi kwa karibu miongo miwili baada ya kuongoza mapinduzi.

Huku kiongozi wa chama cha upinzani cha ANC Jean Pierre Fabre amesema mageuzi hayo ya kikatiba yana lengo moja tu la kumuongezea muda rais, chama tawala kinasema mfumo mpya wa kibunge unaimarisha demokrasia ya Togo.