1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSerbia

Upinzani Serbia wapinga matokeo ya uchaguzi kwa vurumai

25 Desemba 2023

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Serbia wamekabiliana na wafuasi wa upinzani mjini Belgrade wakati wa maandamano yaliyochochewa na madai ya udanganyifu kwenye uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa.

https://p.dw.com/p/4aY92
Serbia I Maandamano mjini Belgrade
Polisi wa kutuliza fujo nchini Serbia wakiwakabili wafuasi wa upinzani mjini Belgrade.Picha: Darko Vojinovic/AP/picture alliance

Maafisa wa usalama walitumia gesi ya kutoa machozi kuwadhibiti waandamanaji waliokuwa wakitumia mawe na milingoti ya bendera kupasua vioo vya majengo hayo ya utawala. Wafuasi hao wa upinzani wanalalamika kuhusu tuhuma za wizi na udanganyifu katika uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa uliofanyika Disemba 17.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonesha chama cha rais Aleksandar Vucic wa nchi hiyo cha Serbia Progressive kimenyakua ushindi wa viti vingi vya bunge la taifa pamoja na serikali za miji ikiwemo mji mkuu, Belgrade. Upinzani unasema umeporwa ushindi kwenye matokeo ya uchaguzi wa mji mkuu.

Rais Vucic ameyataja maandamano ya leo usiku kuwa  jaribio la kuipindua serikali na ni njama kutoka mataifa ya kigeni. Hata hivyo kiongozi huyo hakutoa ushahidi wowote kuhusu madai hayo.