Upinzani Ujerumani wataka wahamiaji haramu wadhibitiwe
23 Januari 2025Matangazo
Weidel, mgombea wa ukansela kupitia AfD, katika uchaguzi wa Februari 23, amesema ni lazima kambi ya kihafidhina ya CDU/CSU iachane na msimamo wake wa kutokushirikiana na chama hicho cha msimamo mkali wa kulia ili kupitisha sheria inayohusiana na "kufungwa kwa mipaka na kuwarejesha wahamiaji haramu.
Waziri Mkuu wa Jimbo la Bavaria Markus Söder naye pia ametaka kufungwa kwa mipaka katika kukabiliana na wahamiaji haramu kufuatia shambulizi hilo lililosababisha vifo vya watu wawili.
Kiongozi huyo wa Chama cha kihafidhina cha Christian Social Union (CSU) katika jimbo hilo, amesema kauli mbiu yao ni lazima iwe usalama kwanza.